Isaiah 58:1-6

Mfungo Wa Kweli


1 a“Piga kelele, usizuie.
Paza sauti yako kama tarumbeta.
Watangazieni watu wangu uasi wao,
na kwa nyumba ya Yakobo dhambi zao.

2 bKwa maana kila siku hunitafuta,
wanaonekana kutaka kujua njia zangu,
kana kwamba walikuwa taifa linalotenda lililo sawa,
na ambalo halijaziacha amri za Mungu wake.
Hutaka kwangu maamuzi ya haki,
nao hutamani Mungu awakaribie.

3 cWao husema, ‘Mbona tumefunga, nawe hujaona?
Mbona tumejinyenyekeza, nawe huangalii?’

“Lakini katika siku ya kufunga kwenu, mnafanya mnavyotaka
na kuwadhulumu wafanyakazi wenu wote.

4 dKufunga kwenu huishia kwenye magomvi na mapigano,
na kupigana ninyi kwa ninyi kwa ngumi za uovu.
Hamwezi kufunga kama mnavyofanya leo
na kutazamia sauti zenu kusikiwa huko juu.

5 eJe, hii ndiyo aina ya mfungo niliouchagua,
siku moja tu ya mtu kujinyenyekeza?
Je, ni kwa kuinamisha kichwa chini kama tete,
na kwa kujilaza juu ya nguo ya gunia na majivu?
Je, huo ndio mnaouita mfungo,
siku iliyokubalika kwa Bwana?


6 f“Je, hii si ndiyo aina ya mfungo niliyoichagua:
kufungua minyororo ya udhalimu,
na kufungua kamba za nira,
kuwaweka huru walioonewa,
na kuvunja kila nira?
Copyright information for SwhKC